new_red KARIBU UPAKUE FOMU KWA MAHITAJI MBALIMBALI:new_red MAOMBI YA NAFASI KATIKA SHULE; new_redMirathi / Urithi na Kununua / Kuuza KIWANJA BOFYA HAPA KUZIPATA new_red
UWATA GLORY SOUNDS STUDIO (UWATA GSS) ilizinduliwa rasmi Oktoba 2011, japo mchakato wa uanzishaji wake ulizinduliwa tarehe 15 Novemba 2009 kwa kuwekewa kamati maalumu ya kushughulikia mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Bwana la kila tawi (Faragha) kuwa na mradi wa uhakika.Tangu wakati huo Kamati hiyo maalumu imeendelea na taratibu za kuendesha mradi huo, mwanzoni ilibidi eneo linunuliwe pamoja na jumba lisilokamilika toka kwa mpendwa mwenzetu naye kuhamishiwa na kujengewa nyumba mahali pengine kwa makubaliano maalumu. Baada ya hatua hiyo kukamilika ndipo ujenzi wa jengo la studio ulipoendelea na hata wakati huu ujenzi unaendelea kwa hatua nyingine. Mradi huu kama tulivyoeleze hapo juu ni wa tawi la Bethania lililoko Tabata Dar es salaam ingawa kwa jinsi ulivyo umebeba sura ya kitaifa.
UWATA GSS ipo eneo la Tabata Machimbo- Mtaa wa Mwangoka; huko pakifahamika zaidi kama kwa Walokole. Mwelekeo kutoka Ubungo au kona yeyote ya jiji la Dar es salaam; panda magari yaishiayo kituo cha Tabata Kimanga, ndipo uchukue usafiri wowote ukieleza kuwa unaelekea Tabata Machimbo- Mtaa wa Mwangoka; huko pakifahamika zaidi kama kwa Walokole, ni umbali wa kama mita mia nane (800) toka kituo cha Tabata Kimanga.
Katika kazi zote hilo ndilo eneo lililo na changamoto kubwa, kwani wataalamu wetu tuliowafahamu hawakuweza kufikia viwango vinavyohitajika kufanya kazi katika mazingira ya kisasa yenye ushindani.
Kukabiliana na changamoto ya viwango, Kamati ya studio imeweka mpango mkakati wa kusomesha wataalamu wetu kwa awamu. Na kwa sasa wanaohudumu katika studio ni vijana wetu waliopata uzoefu wa karibu miaka minne toka kwa mtaalamu tuliyekuwa naye. Ikumbukwe kuwa fani kama za sanaa na muziki hazikuwa zikitolewa katika vyuo vyetu na hivyo kupelekea kutokuwapo kwa wataalamu wake.

UWATA GSS imefanikiwa kununua vifaa vya kisasa vya studio, ingawa kadri teknolojia inavyokuwa basi itafikia wakati vitanunuliwa vingine, ila kwa sasa ndiyo vilivyopo sokoni na pengine kusiwe na studio nyingine yenye vifaa kama hivyo kwa hapa Tanzania labda nje ya nchi.Picha za baadhi ya vifaa hivyo zinaonekana hapo mwanzoni.
Kazi hiyo tayari inaendelea na hata baadhi ya kwaya zetu zimekwisha kurekodi. Changamoto kubwa pia ipo katika idara hii kwani waimbaji wengi huwa na maandalizi duni yanayopelekea kutofikia viwango. Hata waimbaji wetu wanapaswa kuzingatia maandalizi yenye viwango kwani hata kuimba lazima kufanyike kwa ustadi na usanifu mkubwa kama alivyo imba mfalme Daudi. Pia ili kazi zetu ziweze kuuzwa zapaswa kufikia viwango vya ubora.Tukumbuke kuwa moja ya sifa ya studio ni kama inazingatia viwango vya ubora na ndicho alichohimiza mtaalamu tuliye kuwa naye kwani kama si viwango vyake vya ubora asingalitafutwa.
Kazi hii imeanza na kwa mwanzo wake tumepata changamoto iliyozaa upanuzi wa mradi. Ni kwamba tumepata ugumu wa kuzitangaza kazi za wateja wetu kupitia redio na runinga zilizopo kwa kuwa wamekuwa wabaguzi wa kutozipa nafasi kazi zetu, hivyo Kamati imeanza mkakati wa kuwa na kituo cha Redio na baadaye Runinga ili kufanikisha azma ya utangazaji wa kazi za wateja wetu na hatimaye usambazaji kuwa rahisi.
Kazi hii imeanza na tayari, baadhi ya wateja wetu kazi zao zimekamilika. Tumeongeza vifaa vya kitengo hicho cha video kutokana mahitaji ya wateja wetu.
Kutokana na hali iliyojitokeza ya wateja wetu wakati mwingi kushinda hapa studio kwa muda mrefu, na wakati wote migahawa na hoteli zikiwa mbali,wateja hao wameshinda bila kula na hivyo kupunguza utayari wa kufanya kazi waliyojia. Kwa kutambua umuhimu wa wateja na muda wa kufanya kazi zao kwa ufanisi basi tumefungua mgahawa (kantini) inayoweza kuhudumia watu zaidi ya arobaini kwa wakati mmoja. Katika mgahawa huu tunahudumia kwa bei ya kawaida na huduma hutolewa kwa watu wote hata kama hukuja kwa ajili ya kurekodi.
  • Kuwa na kituo cha Redio na Runinga

Waweza kuwasiliana nasi kupitia njia hizo hapo chini:

  • Simu no: 0756016816
  • Barua pepe:studio@uwata.or.tz
  • Nukushi no:

KARIBUNI UWATA GLORY SOUNDS STUDIO KWA VIWANGO BORA VYA KAZI ZENU!!!