Lengo la awali la UWATA ni kuamsha Wakristo na kila mmoja alalaye dhambini! (Warumi 13:11-14). La pili ni kuhubiri neno
la Mungu kwa watu wote na kufanya jitihada (ikiwamo kufundisha, kuhimiza na kushauri) kuhakikisha kwamba matunda
(wale walio tubu dhambi na kuziacha) wakae katika utauwa kumsubiri Bwana harusi, Yesu Kristo. Hii imefanikiwa
kupitia kukusanyika kila iitwapo leo, (Waebrania 3:13, 10:25). Pia tunatoa huduma mbalimbali katika jamii kama
elimu, afya na kushiriki katika utunzaji wa mazingira.