Tunamshukuru Mungu kazi ya uinjilishaji imeendelea vizuri ndani ya kanisa kwa kuwatumia watenda kazi wa Kanda na
Walezi kwa ukaribu sana. Kila kanda imejipangia ratiba ya kutembelea makanisa katika kanda husika na kwa taarifa
za hivi karibuni katika kanda mbalimbali kumefunguliwa matawi mapya. Lengo ni pamoja na kuimarisha makanisa na
kufungua matawi mapya baada ya kufikisha ujumbe wa injili ya Yesu Kristo katika maeneo yasiyofikiwa. Kwa upande
mwingine, Walezi kwa miaka ya hivi karibuni wameweza kutembelea makanisa karibu yote kwa lengo la kuhimiza ujumbe
wa mwaka pamoja na mafundisho ya ziada yaliyofunuliwa kwao kama mafundisho ya kuwa na huruma kwa wenye shida na pia
mafundisho ya kulirudisha kanisa katika msingi wa kweli wa "kutubu dhambi za asili, kuziacha, kusamehewa na
kutembea katika msamaha" yakiwa ni mafundisho ya msingi toka kwa mwasisi wa UWATA.